Shaaban Robert: Mapenzi Bora

Na MAKTABA

Imepakiwa - Thursday, January 24  2019 at  11:55

Kwa Muhtasari

Kitabu hiki kiliandikwa na Marehemu Shaaban Robert mwaka 1958.

 

HIKI ni kitabu chenye mashairi kilichoandikwa chenye beti 690. Kitabu hiki kiliandikwa na Marehemu Shaaban Robert mwaka 1958.

Shaaban Robert alisema kusudi la kuandika kitabu hiki ni “kuandalia mahitaji ya watu waliofikia fahamu ya kuwaza na kuhoji neno au kitu au tendo kwa akili. 

Watu ambao wana dhana ya kuwa mapenzi si kitu cha maana wanaonywa katika kurasa hizi kuwa wanapatwa na hasara kubwa. Baadhi ya watu hudai kuwa mapenzi ni karaha kuzungumzwa. Yafaa watu waelewe kuwa Kiswahili si lugha ya watoto na vitabu vya chuoni tu. Huweza kuzungunza biashara dini, sheria na mapenzi

Wale wasemao kwamba mapenzi ni karaha hawawafunzi wazazi kukaa vyema na watoto  wao wala watoto kuwa wema na amani kwa wazazi wao. Hawawafunzi watu kuwajibu wa kutegemeana katika dunia. Huharibu unoja na ujirani, uaminifu na urafiki

Mapenzi ni moja ya mambo yaliyo muhimu na wajibu kwa mtu katika maisha yake.”

Katika tenzi alizoandika Shaaban Robert kuhusu “Mapenzi Bora” anaanza utenzi wake kama ifuatavyo:

1.   JINA limetakadimu,

      Na moyo umeazimu,

      Kabla juma kutimu,

      Kuandika simulizi.

 

2.   Pindi nikiwa mzima,

Muda ukipita juma

Tawapa habari nzima,

Nikijaliwa pumzi.

 

3.   Nikifunguliwa heri,

 Na nguvu ya kufikiri,

Nitatunga kwa shairi,

Wimbo tunu nchi hizi.

 

4.   Hata kama siku hizi

Mwli wangu una ganzi,

Kabla robo  a mwezi,

Makala yatabarizi.

 

5.   Yatabarizi makala,

Kwa uwezo wake Illah,

Apaye watu chakula

Uzima na usingizi

 

6.   Toka kalamu kushika,

Arobaini miaka,

Bado sijapumzika,

Na kuiacha siwezi.

 

 7. Kutunga na kutangua

Kuwaza na kushangaa,

Sijakoma robo saa,

Kila siku nina kazi.

 

8.   Kwa wino na kalamu,

Kusoma na kudurusu,

Macho yangu nayahisi,

Kuona yana tanzu.

 

9.   Kuona natatizika,

Kwa nuru kunitoweka,

Na kila nikiandika,

Herufi si wazi.

 

10.  Macho yamejaa kiwi,

Herufi hayatambui,

Walakini kazi hii,

Kuiacha sifanyazi.

 

11.   Japo dhaifu wa mwili,

Napenda kutawalaki,

Kazi hii ya asili,

Na kuitupa siwaze.

 

12.       Na kuacha sikubali,

Siwezi kwa kila hali,

Kila asili ni mali

Kuacha haipendezi.

 

13. Kitupa neno gumu,

Na kama litalazimu

Tadhuriwa na mizimu

Ninazo fikra hizi.

 

14. Jadi itanisumbua,

Nijutie kuzaliwa,

     Hapa katika dunia,

     Maisha yatanihizi

 

15. Sio masihara jadi,

Ni kitu hakina budi,

Kutunzwa kwa jitihada,

Moyo wangu wamaizi’

 

16. Sisi tusio na kitu,

Katika maisha yetu,

Jadi mali bora kwetu,

Kudharau ni upuzi.

 

17. Si tayari kutupa,

Furaha na kunenepa,

Hata kama kutanipa,

Na ufalme na enzi

 

18. Ningestahabu jadi,

Kuliko kupata sudi,

Ya dhahabu na makidi,

Kukidhia matumizi

 

19.   Nilitupa kijana,

Wakati akili sina,

Sasa sikubali tena,

Nijapopewa feruzi.

 

20.    Kabla ya kutumika,

  Maandiko Afrika, 

          Kuimba tulisifika,

          Kwa nyimbo na tumbuiz.

     

21. Nilipokuwa kijana,

    Ingawa nilikazana,’

    Kama hili sikuona,

   Naliona siku hizi

     22.Lingefanya majilio,

     Lingefanya majilio,

      Wakati nguvu ninayo,

       Ningeacha nyuma nyayo,

      Ambazo hazipotezi.

 

23. Ningewachia alama

      Waone wajao nyuma,

      Asaa ikiwa njema,

      Kwao kama maongozi.

24. Yana ajabu maisha,

     Yakikaribia kwisha

     Ndipo yanapoamsha,

    Fani mashazi mashazi

 

25. Na jua letu likichwa

Na mvi katika kichwa,

Mioyoni twachokochwa,

Haja ztu hazituzi.

 

26. Wakati wa kwenda mbio,

  Maisha kwenye kituo,

Twapata wakati huo,

Maono juzi kwa jozi,

 

27. Na ijapo mansubu,

Akili ya kuratibu,

Mambo kwa utaratibu,

Mwili hauwezi kazi.

 

28. Tunapojiwa na lubu,

Na akili mjarabu,

Wali twaona tabu,

Kuumia hatuwezi.

 

29. Na tukiwa taabani,

Hatuna nguvu mwilini,

Ndipo ijapo kichwani

Akili iliyo razi

 

30. Maisha yetu mafupi

Na sijui twende wapi,

Mambo yatakuwa vipi,

Kama huna sifanyizi.

 

31. Unaishi kwa kuhama,

Lazima nifanye hima,

Mama kifo daima,

Hutokea kama mwizi.

32. Dibaji ikome hapa,

Kwa sababu nina pupa,

Na haraka ya kuwapa,

Habari bila ajizi.

 

33. Kama nitaajiizika,

Na mambo yatajizika,

Yawe dhiki kuchimbuka,

Yasumbue wachimbuzi.

 

34. Ni heri nifululize,

  Nisikwae niteleze, 

Kila baya nilmeze,

Jema niwape wapenzi.

 

35. Kisa cha huu utenzi,

Ni kuyahami mapenzi,

Hata nikiwa mpuzi,

Nia hii sigeuzi.

 

36. Nia yangu sigeuzi,

Sitishwi na pingamizi,

Nitanena waziwazi,

Niachie waamuzi.

 

37. Wimo wangu taachia,

Watu wema kuamua,

Sina haja kuzuia,

Kuitisha maamuzi

 

38. Taachia wenginewe,

Penye kosa wakosoe,

Lakini mimi mwenyewe,

Kufanya hiyo fauzi.

 

39. Ni upuuzi kukzshifu,

Natenda kwa takilifu,

Walakini kukashifu,

Mambo nina mazoezi.

 

40. Mapenzi nitayasifu

Mnaka siku ya ufu,

Maana ndio turufu,

Kwangu iliyo azizi.

 

41. Sifa zake nitapanga,

Kwa fikira za kuwanga,

Na maneno yenye anga,

Yatajaa beti hizi.

 

42. Mapenzi nitayasifu,

Mnaka siku ya ufu,

Maana ndiyo turufu,

Kwangu iliyo azizi.

 

41. Sifa zake nitapanga,

Kwa fikira za kuwanga,

Na maneno yenye anga,

Yatajaa bezi hizi.

 

42. Beti nitazishibisha,

Maneno ya mshawasha,

Mema kwa kuchangamsha,

Kama siki  kwa mchuzi.

 

43. Maneno niliyo nayo,

Nitafuma yawe nguo,

Niupambe wimbo huo,

Kama mwili na mavazi.

 

44. Nitaupamba kwa pambo,

Wimbo upendeze umbo,

Walie wivu warembo.

 

45. Wivu walie Ulaya,

Watu welewa Sanaa,

Kila pembe ya dunia,

Jumla watunga tenzi.

 

46. Mapenzi kwangu uhai,

Kila mara hukinai,

Kama ninywa divai,

Baridi katika kuzi.

 

47. Kama ninywae asali,

Tamu kama asili,

Au kitu cha halali,

Kipendezacho  Mwenyezi.

 

48. Atafutae malau,

Si mwerevu ni bahau,

Kayavunja kwa nahau,

Mapenzi mtu hawezi.

 

49. Anambaye hapendi,

Njia moja naye sendi,

Nashuku kunywa mtindi,

Maneno mema hawezi.

 

50. Nahofu kanywa kangara,

Kileo chenye madhara,

Na fikira zimegura,

Kuzingatia hawezi.

 

(Itaendelea)