http://www.swahilihub.com/image/view/-/3803422/medRes/1556717/-/7fyldqz/-/ajika.jpg

 

Marufuku kukata tamaaMarufuku kukata tamaa

2jiajiri

Rais Uhuru Kenyatta akiwa na baadhi ya viongozi kwenye hafla ya kuwashajiisha vijana chini ya mpango wa benki ya KCB wa 2jiajiri kutia bidii Februari 7, 2017. Picha/PSCU 

Na JENITHA WALTER

Imepakiwa - Tuesday, April 10  2018 at  15:07

Kwa Muhtasari

Maisha daima hayalingani jinsi ambavyo vidole havitoshani.

 

KAMA vilivyo vidole ambavyo havilingani ndivyo maisha hayalingani.

Kuna watu ambao wamefanikiwa kimaisha na wengine wakiwa na hali mbaya kiuchumi. Kuna msemo uliibuka ambao binafsi ninaamini kama tukiufanyia kazi unaweza kutusogeza sehemu tulipo na kutupeleka hatua nyingine ya maendeleo zaidi, msemo huo ni ‘Kuzaliwa maskini ni kudura za Mwenyezi Mungu ila kufa maskini ni uzembe wako’. Msemo huu tukiuangalia kwa jicho pevu unahamasisha watu wasiridhike na maisha waliyonayo hivyo wapambane kutafuta ili wafanikiwe.

Katika kutafuta sio wote ambao wanapenda kuona mafanikio yako. Kama Bahati Bukuku alivyoimba ‘unapoianza safari wanakutia moyo, unapoonesha mafanikio wanainua vikwazo’, sio wote ambao wanapenda usonge mbele kimaisha. Unaweza kumshirikisha mtu kuhusu jambo lako unalotaka kufanya badala ya kukutia moyo na kukupa ujasiri kuwa unaweza, ndio anakuwa wa kwanza kukukatisha tamaa kuwa ‘sidhani kama utaweza’.

Katika umri wangu huu mdogo nilionao, nimejifunza mambo mengi na jambo la msingi linaloniongoza ni ‘kutokata tamaa’. Ninapowaza au kutaka kufanya jambo sitangulizi kushindwa bali kushinda. Kabla ya kuanza kufanya jambo lolote ukitanguliza wasiwasi sio rahisi kufanikiwa kwani hutajiamini katika jambo unalolifanya.

Napenda kuwasihi ndugu zangu kuungana nami katika kampeni ya kupiga marufuku kukata taamaa kwani ni adui wa maendeleo. Kauli mbiu ni USHINDI DAIMA.