Mipaka kati ya Semantiki na Pragmatiki

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Thursday, February 1  2018 at  06:17

Kwa Muhtasari

Hapa tunachohitaji kujiuliza ni kwamba kuna mpaka dhahiri kati ya Semantiki na Pragmatiki au mipaka iliyopo ni ya kiuchambuzi tu?

 

HAPA tunachohitaji kujiuliza ni kwamba kuna mpaka dhahiri kati ya Semantiki na Pragmatiki au mipaka iliyopo ni ya kiuchambuzi tu?

Je, watu wanapozungumza hufikia wakati wanajua kwamba sasa naingia Pragmatiki?

Pengo la Kileksika

Ni wazi kwamba hakuna lugha yoyote duniani ambayo inajitosheleza kimsamiati kuweza kuelezea kila dhana.

Hivyo kila lugha ina pengo la kileksika. Swali la kujiuliza hapa sasa ni je, lugha inapokosa msamiati wa kutaja dhana fulani kuna mbinu gani inatumika kutaja dhana hiyo? Mbinu hiyo nani aliiweka?

Kutokana na hoja tulizoainisha ni wazi kwamba si rahisi kujishughulisha na Semantiki na Pragmatiki katika uhalisia wake bali itabaki kuwa katika nadharia tu.

 

Uchambuzi wa sinonimia

Sinonimia:

Kwa mfano; inua, nyanyua, nyakua

Utofauti: 

 Inua ni wakati sehemu tu ya kitu inakuwa juu wakati nyanyua sehemu yote ya kitu inakuwa juu na hakuna sehemu itabaki kuwa chini lakini nyakua ni sehemu yote ya kitu itakuwa juu lakini tendo linafanyika kwa haraka sana.

 

Ulinganisho:

Maneno yote haya humaanisha kuweka juu kitu 2.

 

Sinonimia:

Mfano; Cheo, Madaraka na Wadhifa

 

Utofauti: 

Cheo ni ngazi, ajira au madaraka. Ni ngazi ya kimuundo ambayo hutegemea elimu na ufanisi wa mtu lakini madaraka ni nguvu za kiutendaji kazi alizo nazo mtu kutokana na cheo chake lakini wadhifa ni haki inayofungamana na madaraka aliyo nayo mtu kutokana na cheo chake. Ni hadhi ya kijamii.

 

Ufanano:

Maneno yote haya yanahusu mtu kupata heshima fulani

 

Sinonimia:

 

Mfano: Pikipiki na bodaboda

 

Utofauti: 

Pikipiki ni kwa ajili ya matumizi ya jumla lakini bodaboda ni kwa ajili ya biashara (kubeba abiria)

 

Ufanano: 

Zote hutumia magurudumu mawili na mota ya kutumia mafuta.

Zote ni pikipiki lakini si pikipiki zote ni bodaboda

 

Sinonimia:

Uso na Sura

Utofauti: 

Uso ni halisi ni kitu kinachoshikika (complete) lakini sura ni dhahania na haishikiki.

 

Ufanano: 

Zote hurejelea sehemu ya mbele ya kichwa cha mnyama (hasa binadamu)

 

Sinonimia:

Shimo, tobo na tundu

Ufafanano wake ni uwazi tu. Kwamba vyote hivi vinazungumzia uwazi. Lakini kuna totauti zake.

 

Fahiwa ya mwelekeo.

Shimo lazima uelekee chini ambapo tobo na tundu si lazima uwazi wake uelekee chini lakini kwa shimo ni lazima