http://www.swahilihub.com/image/view/-/4895246/medRes/2197893/-/1a5cdcz/-/wangari.jpg

 

Dhana za wataalamu mbalimbali kuhusu Nadharia kama mwongozo

Mary Wangari

Mwandishi Mary Wangari. Picha/MAKTABA 

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Tuesday, January 29  2019 at  11:50

Kwa Muhtasari

  • Hassan Msami katika tahakiki yake ya Malenga wa Vumba (1982) alibainisha sifa za bahari 14 kimuundo

  • Bahari Hizo ni: kikai, msuko, sakarani, mtiririko, ukara, ukaraguni, kikwamba, msuko wa kikai, tathlitha, tarbia, takhmisa, ukemi, pindu na utenzi

 

SHIHABUDDIN Chiraghdin aliyaainisha mashairi ya Ahmad Nassir katika vitengo vinne ambavyo ni:

i. Mbinu za Lugha

ii. Mawazo na Maliwazo

iii. Baina va Mume na Mke

iv. Majonzi na Makiwa.

Uainisho huu ni ithibati tosha kuonvesha kwamba si lazima ushairi wa Kiswahili ufikiriwe kimuundo kila mara mijadala va kinadharia inapozuka.

Diwani ya Ustadh Nyamaume nayo iliandikiwa uhariri wake na Abdilatif Abdalla. Abdalla anashabihianana Chiraghdin katika kubainisha ushairi wa Nvamaume kimaudhui.

Hata hivvo, rngawanvo wa Abdilatif haulandani reale kwa ya pili na uainishaji wa Shihabuddin Chiraghdin. Mashairi yake yanahusu:

i. Kuusemea Ushairi

ii. Malimwengu

iii. Kushauri na Kunasihi

iv. Kuimbana Kishairi

v. Kufumba na Kupiga

vi. Mifano na Kutoa Heko

 Kwa mantiki hii tunaweza kuhitimisha  kuwa uainisho wa ushairi wa Kiswahili kimaudhui ni rnnyumbufu kwa vile maudhui rnapva vanaweza kuibuka na kusababisha uundaji wa makundi rnapva va ushairi kimaudhui. Kwa upande mwingine mijadala kuhusu muundo wa shairi la Kiswahili ilianza kudhihirika kwa makali baada va kutungwa kwa diwani va Euphrase (1974), Kahigi na Mulokozi (1976) na Mulokozi na Kahigi (1979).

Shihabuddin Chiragdin alilihisi wimbi la watunzi hawa ambao kwa wakati huo walikuwa wakereketwa kiasi na kusemezana na ushairi wao katika utangulizi wa Malenga wa Mrima (1977).

Sasa mashairi hayakuainishwa kimaudhui kama ilivvofayvwa kinagaubaga katika Malenga wa Mvita.

Mhariri wa Malenga wa Mrima alijipa fursa va kushambulia mashairi vasivofuata arudhi.

Jambo hili lilishadidiwa na Hassan Msami katika tahakiki yake ya Malenga wa Vumba (1982).

Katika tahakiki hivo, alitambua kueleza sifa za bahari 14 kimuundo. Bahari Hizo ni: kikai, msuko, sakarani, mtiririko, ukara, ukaraguni, kikwamba, msuko wa kikai, tathlitha, tarbia, takhmisa, ukemi, pindu na utenzi.

Katika mazingira va sanaa za Kimagharibi nadharia kama mwongozo inadhihirika katika matamshi va Aristotle katika tahakiki vake va Poetics (1965).

Aristotle aliorodhesha na kufafanua sifa na mazoea ya Wayunani kuhusu utunzi wa tamthilia.

Alifanva hivvo bila kuwashinikiza watunzi na wahakiki kufuata aliyoyashuhudia.

Baruapepe ya mwandishi: marya.wangari@gmail.com

Marejeo:

Mulokozi, Mugyabuso & Kahigi K.(1979). Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.

Njogu, K. & R.M. Wafula (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Shihabuddin, C. (1970). Utangulizi: Malenga wa Mvita. Nairobi: Oxford University Press.

Je, una swali, maoni au mapendekezo kwa Swahili Hub? Baruapepe ni: swahilihub@ke.nationmedia.com