Nadharia ya mawasiliano kama taaluma ya kiakademia

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Tuesday, November 13  2018 at  07:24

Kwa Muhtasari

Je wajua kwamba mizizi ya mimea huweza kuwasiliana na bakteria na wadudu walio kwenye ardhi.

 

KATIKA makala ya iliyotangulia tulitjadili kuhusu nadharia ya urekebishaji pamoja katika mawasiliano.

Pia tuliangazia kuhusu mawasiliano baina ya wanyama ambapo tulijadili kwa kina kuhusu utafiti huo.

Katika makala ya leo tutagusia kwa ufupi kuhusu mawasiliano ya mimea jinsi ifuatavyo:

Mawasiliano ya Mimea

Mawasiliano katika mimea hutokea na kuonekana  ndani ya mmea wenyewe kupitia seli za mmea, kati ya mimea ya aina moja au inayohusiana katika kiitengo chake na kati ya mimea na viumbe visivyo hai, hasa katika sehemu ya mizizi. 

Mizizi ya mimea huweza kuwasiliana na bakteria na wadudu walio kwenye ardhi.

Mimea pia kuwasiliana kupitia kwa mivuke katika kisa cha tabia za wakati wa mashambulizi na wanyama wala mimea ili kuonya mimea jirani.

Vilevile, mimea hiyo hutoa mivuke ya kuvivutia vimelea ambavyo huwashambulia wale wanyama. Katika misimu ya dhiki mimea inaweza kubadilisha kodi ya kinasaba iliyorithi kutoka kwa  wazazi wao na kurudi kwa ile ya mababu zao.

Mitagusano hii inayohusisha ishara na inayoongozwa na kanuni za kisintaksia, kipragmatiki na kisemantiki hutokea kwa sababu ya "mfumo uliogatuka.

 

Mawasiliano kama Taaluma ya Kiakademia

Mawasiliano kama taaluma yanayofahamika pia kama komunikolojia yanahusisha njia zote tunazozitumia kuwasiliana.

Komunikolojia hivyo basi inahusisha sehemu kubwa ya utafiti na maarifa.

Taaluma ya mawasiliano inahusisha mawasiliano ya kimaongezi na yasiyo ya kimaongezi. Mkusanyiko wa maarifa kuhusu mawasiliano umewakilishwa na kufafanuliwa katika vitabu, machapisho ya kielektroniki, na majarida ya kiakademia.

Katika majarida, ripoti za kitafiti ndizo matokeo ya tafiti ambazo ni msingi wa uelewa, unaoendelea kupanuka, wa jinsi binadamu wanavyowasiliana.

Mawasiliano hufanyika katika ngazi tofauti katika njia mbalimbali, na kwa viumbe wengi, na vilevile kwa mashine fulani.

Baadhi ya taaluma za utafiti , ikiwa siyo zote, hutenga sehemu ya mafunzo yake kwa mawasiliano, hivyo basi wakati wa kuzungumza kuhusu mawasiliano, ni muhimu sana kuwa na uhakika kuhusu nyanja ya mawasiliano inayozungumziwa.

Ufafanuzi wa mawasiliano hutofautiana sana, baadhi yake ukitambua kwamba wanyama wanaweza kuwasiliana na wenzao na binadamu pia, na baadhi ni finyu zaidi, ukihusisha binadamu katika mitagusano ya kibinadamu iliyo na maana.

Marejeo:

Warwick, K, Gasson Hutt, B, Goodhew, I,Kyberd P,  Schulzrinne, H na Wu, X: "Thought Communication and Control: A First Step using Radiotelegraphy", IEE Proceeedings on Communication, 151 (3), pp.185-189, 2004

Mehrabian na Ferris (1967). "Inference of Attitude from Nonverbal Communication in Two Channels". Katika: The Journal of Counselling Psychology Vol.31, 1967, pp.248-52.

Witzany, G. (2006 Plant Communication from Biosemiotic Perspective. Plant Signaling na Behavior 1 (4): 169-178.