http://www.swahilihub.com/image/view/-/2983618/medRes/982966/-/12bbn23z/-/DNNYERIUGALI2202A.jpg

 

NJAA INAPONZA

Ugali

Ugali ukiwa kwenye sahani. Picha/JOSEPH KANYI 

Na SHAABAN MAULIDI

Imepakiwa - Tuesday, January 29  2019 at  16:21

Kwa Muhtasari

Hala hala e jirani, tega sikio sikia,

Shauri yako jirani, njaa yako inaponza. 

 

HALA hala e jirani, tega sikio sikia, 
Kuzaliwa masikini, wala siyo wa kufia, 
Usiende tatizoni, eti kisa yako njaa, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

 

Sikio weka kichwani, katu siweke tumboni, 
Itumie yako mboni, kuyatazama angani, 
Uonavyo machoni, si vyote vyenye thamani, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

 

Wivu wako ni kidonda, ushiriki utakonda, 
Sipendi njia mlenda, kuteleza kisha kwenda, 
Usije tokwa udenda, ukawa kipendapenda, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

 

Umezaliwa kidume, shika jembe ukalime, 
Juhudi tena jitume, ndiyo sifa ya kiume, 
Tamaa tena ukome, kazini ufanye shime, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

 

Usije shikwa tamaa, kisa pesa umekwama, 
Sababu unayo njaa, likakuteka jimama, 
Kwa pesa kukuhadaa, penzini kuja kuzama, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

 

Ewe binti malikia, epuka sana mabuzi, 
Usipende kimbilia, kujitoa kimapenzi, 
Kisa pesa kupokea, mwili ukaache wazi, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

 

Utaja pata maradhi, sababu kupenda pesa, 
Mwili wako uhifadhi, usipende kujitesa, 
Usijejishusha hadhi, ukafa kisa anasa, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

 

Usijeacha mbachao, kwa msala upitao, 
Shikeni mlionao, msitake wapitao, 
Pendeni zuri chaguo, tamaa mwisho kilio, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

 

jambazi, ama uwe muuaji, 
Njiani uvunje nazi, ama uwe muwangaji, 
Hata kama kiongozi, utakuwa mfujaji, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

 

huwa inaponza, shika sana shikilia, 
Usije kuendekeza, njiani wakakutoa, 
Jifunze kujiongeza, usijeponzwa na njaa, 
Shauri yako jirani, njaa yako inaponza.

Jina la mtunzi: Shaaban Maulidi.
Jina la utungo: Kazi na bata.
Rununu: +255763902318/ +255718526159.