http://www.swahilihub.com/image/view/-/3208016/medRes/1329899/-/k2ingwz/-/tfJuhaKalulu1.jpg

 

BURIANI KALULU

Edward Gitau

Marehemu Edward Gitau almaarufu kama Juha Kalulu wakati akifanya kazi Machi 9, 2010 katika Jumba la Nation. Gitau alifariki Mei 17, 2016. Picha/FREDRICK ONYANGO 

Na RICHARD MAOSI

Imepakiwa - Wednesday, June 8  2016 at  00:23

Kwa Muhtasari

Mchoraji wa vibonzo, kwa miaka na mikaka,

Mlaze pema peponi, Mzee Juha Kalulu.

 

MCHORAJI wa vibonzo, kwa miaka na mikaka,
Mwasisi tangu mwanzo, gazetini mtajika,
Mchoraji wa michezo, ya kuigiza hakika,
Mlaze pema peponi, Mzee Juha Kalulu.

Leo ninamsifia, madhali alinipunga,
Ni mlezi wa sanaa, kwao alio wapunga,
Michoro alitumia, amali zilipotinga,
Mlaze pema peponi, Mzee Juha Kalulu.

Dunia tena hayupo, amerudi kwa manani,
Kumbukizi bado zipo, amini usiamini,
Nafusi japo haipo, twaenzi zake nishani,
Mlaze pema peponi, Mzee Juha Kalulu.

Amekuwa ndiye fundi, stadi mkubwa sana,
Miongoni kwenye kundi, alibainika bwana,
Hasauliki hagandi, tutamuwenzi amina,
Mlaze pema peponi, Mzee Juha Kalulu.

Zimezagaa habari, zizi hizi za tanzia,
Kuhusu mwanahabari, yuyu huyu wa sanaa,
Kwani tunatahayuri, ameondoka dunia,
Mlaze pema peponi, Mzee Juha Kalulu.

Daima umetukosha, tutakukumbuka jama,
Tena ulituchekesha, madhali tunaungama,
Siwezi kukaimisha, japokuwa umehama
Mlaze pema peponi, mzee juha kaluu.

Richard Maosi,

'Amiri Kidedea’

Nairobi.

Imepitiwa na kuthibitishwa na:

Stephen Maina

Dar es Salaam, Tanzania