http://www.swahilihub.com/image/view/-/4890032/medRes/2194553/-/xcsjbwz/-/maria.jpg

 

Sarufi Miundo Virai Zalishi

Mary Wangari

Mwandishi Mary Wangari. Picha/MAKTABA 

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Monday, January 7  2019 at  10:58

Kwa Muhtasari

Katika kipengele cha sarufi miundo virai zalishi muundo wa sentensi huelezwa kwa kuchanganua viambajengo au ukipenda vijenzi vyake.

 

TUMEKUWA tukichambua na kupambanua kuhusu tawi la sintaksia katika Kiswahili.

Hii leo tutaangazia kuhusu kipengele cha sarufi miundo virai zalishi. Katika kitengo hiki muundo wa sentensi huelezwa kwa kuchanganua viambajengo au ukipenda vijenzi vyake. Viambajengo hivi huchanganuliwa hadi kufikia neno moja ambalo hubainishwa kwa kategoria yake ya kisarufi. Uchanganuzi huu wa sentensi huelezwa kwa kanuni ambazo huwezesha kutunga sentensi nyingi zaidi.

Kanuni za muundo virai

Kanuni hizi zinaweza kusawiriwa ifuatavyo:

 

KN = N --- mtoto

Hii ina maana kuwa KN ina N (Kirai Nomino kina kiambajengo kimoja tu ambacho ni nomino). Aidha, hii inaweza kuelezwa kufafanuliwa kwa namna hii:

 

KN

\

 N

\

Mtoto

 

 

Hii ina maana kuwa kirai hiki ni neno moja. Nalo ni ‘mtoto’.

Kirai chenye viambajengo zaidi ya kimoja au chenye maneno zaidi ya moja huelezwa kwa kanuni kama ifuatavyo:

 

KN =N +V au Mtoto mcheshi

Hii ina maana kuwa KN kinaundwa na maneno mawili, yaani ‘mtoto mcheshi’.

Vivyo hivyo kwa Kirai kitenzi (KT)

KT = T anakula

Hapa tunaona kuwa KT ina T yaani ina kiambajengo kimoja tu ‘anakula’. Hii inaweza kuelezwa kwa njia ya matawi pia. Iwapo KT ina viambajengo viwili, muundo wake huelezwa kwa jinsi hii:

 

KT =T +KN. Muundo huu unaelezeka pia kwa njia ya matawi hivi:

 

KT

 

 T KN

 N

 anakula chakula

 

Vivyo hivyo kwa:

KV =V au KV =V +E,

 

KV

 

 V E

 mdogo sana

 

KE = E au KE =E +E

 

 KE= E+ E

taratibu mno

 

KH=H au KH =H +KN

KANUNI ZA MSINGI ZA MIUNDO VIRAI

Kanuni za miundo virai hujidhihirisha katika sentensi. Kwa mfano, sentensi ifuatayo inaweza kuchanganuliwa kwa kuzingatia kanuni za miundo virai jinsi ifuatavyo katika mfano huu:

 

Mama ameandaa chakula kingi mno.