http://www.swahilihub.com/image/view/-/4842356/medRes/1071616/-/6lavg8z/-/ObamaTabasamu.jpg

 

Sifa badilifu katika nadharia ya mawasiliano

Barack Obama

Aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama atabasamu. Picha/AFP 

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Thursday, November 8  2018 at  12:18

Kwa Muhtasari

Zipo sifa zinazobadilika katika mawasiliano ambazo zinaweza kuashiria aina mbalimbali za maana.

 

KATIKA makala ya leo, tunaangazia mada kuhusu sifa zinazobadilika katika mawasiliano ambazo zinaweza kuashiria aina mbalimbali za maana.

Sifa hizo ni kama zifuatazo:

Kutazama

Hiki ni kiini kikuu cha mawasiliano katika jamii. Kipengele hiki kinaweza kuashiria hisia, wakati wa kuzungumza au kunyamaza, au uhasama.

Aidha, wahusika wanaporudia rudia kutazamana hali hii inaweza kuashiria hisia ya ashiki au uchovu.

Ishara za uso

Ishara hizi zinaweza kujitokeza kama tabasamu, mikunjo ya uso, ishara za nyusi, mathalani kuinua nyusi, kupiga miayo na kusonya kwa madhumuni ya kuwasilisha ujumbe fulani.

Ni muhimu kufahamu kwamba ishara za uso hubadilika mara kwa mara wakati wa mawasiliano na hutiliwa maanani mno na mpokeaji.

Isitoshe, kuna ushahidi kuwa maana ya ishara hizo inaweza kuwa sawa katika tamaduni mbalimbali.

Ishara

Mojawapo ya ishara zinazotumiwa, lakini zisizoeleweka, ni vidokezo katika mwondoko wa mkono. Watu wengi aghalabu wana hulka ya kutumia mara kwa mara miondoko ya mkono wanapozungumza..

Mawasiliano ya kutazama

Haya ni mawasiliano kwa njia ya vielelezo. Kwa maelezo mengine ni hali ya kupitisha mawazo na habari kupitia njia zinazoweza kusomwa au kutazamwa.

Mawasiliano ya kutazama kimsingi yanaweza kuorodheshwa katika vitengo viwili. Mawasiliano haya yanahusisha mifumo kama vile:

  • Raslimali za kielektroniki

  • Miundo ya grafia

  • Rangi

  • Michoro

  • Tipografia

  • Ishara

Sifa ya kipekee ya mawasiliano haya ni kwamba yanategemea tu kutazama. Mawasiliano ya aina hii yanajikita katika dhana kwamba ujumbe unaoonekana ukiunganishwa na maandishi huwa na uwezo mkubwa wa kutaarifu, kuelimisha au hata kumshawishi mtu.

Kwa muhtasari, ishara ni mawasiliano kwa kuwasilisha taarifa kupitia vielelezo.

Ni muhimu kutilia maanani kwamba tathmini ya muundo mzuri wa kutazamwa hujikita kwenye kupima ufahamu na watazamaji na wala si ujumi au upendeleo wa kisanii.

Vilevile, hakuna kanuni bia za uzuru au ubaya. Uwasilishaji wa taarifa kwa kutazama unaweza kuwasilishwa kwa njia anuwai mathalani:

Miondoko ya mwili, video na runinga au kutumia ishara, Lengo kuu katika mawasiliano haya ni katika kuwasilisha michoro, matini picha na kadhalika.zikiunganishwa kwenye maonyesho ya tarakilishi.

Dhana wasilisho la kutazama hutumiwa kurejelea uwasilishaji halisi wa taarifa.

Suala ibuka katika nyanja hii linalenga miundo ya tovuti na matumizi ya graffiti ambapo waundaji graffiti  hutumia mbinu za mawasiliano ya kutazama katika kazi yao.

 

Marejeo

Mehrabian na Ferris (1967). Inference of Attitude from Nonverbal Communication in Two Channels. The Journal of Counselling Psychology Vol.31, 1967, uk.248-52.

Witzany, G. (2006 Plant Communication from Biosemiotic Perspective. Plant Signaling na Behavior 1 (4): 169-178.

Witzany, G. (2007 Applied Biosemiotics: Fungal meddelande. Katika: Witzany, G. (Ed). Biosemiotics in Transdisciplinary Contexts. Helsingfors, Umweb, uk. 295-301.