http://www.swahilihub.com/image/view/-/4890032/medRes/2194553/-/xcsjbwz/-/maria.jpg

 

Tofauti kati ya Teminografia na Leksikografia

Mary Wangari

Mwandishi Mary Wangari. Picha/MAKTABA 

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Monday, January 7  2019 at  13:24

Kwa Muhtasari

  • Leksikolojia ni taaluma ya maneno kwa jumla
  • Leksikografia ni taaluma ya leksikolojia inayohusu utungaji wa kamusi ya maneno ya lugha kwa jumla

 

MTAFITI na mtaalamu Bergenholtz anatupa mwongozo kujua baadhi ya tofauti kati ya Teminografia na Leksikografia.

Tofauti za teminografia na leksikografia.

Teminografia

Leksikografia

1. lugha: hushughulikia lugha ya kitaalamu kwa kuzingatia dhana katika uwanja mahususi wa maarifa

hushughulikia lugha ya jumla kwa kuzingatia maana katika matumizi ya kawaida

 

2. ukusanyaji wa istilahi katika lugha chanzi: hufanywa na wataalamu wa uwanja husika wa maarifa kwa kuzingatia mfumo wa uhusiano wa dhana

maneno ya kamusi hukusanywa na watunga kamusi kwa kuzingatia umbo neno ambapo neno hukusanywa kwa upekee wake kwa kuzingatia walengwa kamusi husika

3. ufafanuzi wa dhana ya istilahi ni elekezi na hufanywa na wataalamu wa uwanja husika wa maarifa

ufafanuzi wa maana ni wa kimatumizi na hufanywa na jopo la watu wenye ujuzi mkubwa wa lugha kimatumizi ambapo miktadha mbalimbali ya kiisimu, kijamii, na kitamaduni ya mahali neno linakotumika, hutumiwa kama msingi wa ufafanuzi wa maana

4. lengo la uundaji istilahi ni kurahisisha mawasiliano ya kitaalamu katika uwanja mahususi wa maarifa baina ya wataalamu wenyewe, wataalamu na wanafunzi wao, na wataalamu na wateja wengine wa maarifa yao

lengo la uundaji kamusi ni kurahisisha mawasiliano ya jumla ya lugha yaani kukuza uelewa wa msamiati wa lugha kwa kuzingatia viwango mbalimbali vya watumiaji wa lugha

5. sinonimi hukusanywa pamoja na kuhusishwa na ufafanuzi mmoja wa dhana

sinonimi huingizwa kama vidahizo tofautitofauti

6. homonimi hukusanywa kama istilahi huru za nyanja tofauti za maarifa

homonimi huingizwa kama kidahizo kimoja na maana zake kutofautishwa

7. istilahi ya neno moja ina dhana pana ambayo inaweza kupewa umahususi kwa kurefushwa kama istilahi ya maneno mawili na zaidi

kidahizo huingizwa kwa upekee wake ambapo vishazi vya zaidi ya neno moja huingizwa tu iwapo vina hadhi ya neno moja kimaana

Baruapepe ya mwandishi: marya.wangari@gmail.com

 

Marejeo

Matinde, R. S. (2012). Dafina ya Lugha Isimu na Natharia. Kwa Sekondari, Vyuo Vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers.

Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa Isimu, Fonetiko, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi Kenya: Longhorn Publishers

 

 

Je, una swali, maoni au mapendekezo kwa Swahili Hub? Tuandikie kupitia baruapepe: swahilihub@ke.nationmedia.com