Ueneaji wa Wabantu kutoka Kongo hadi Afrika Mashariki

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Tuesday, November 27  2018 at  10:39

Kwa Muhtasari

Hapa tunafaa kuzingatia umuhimu wa nadharia kwamba Kiswahili ni lugha ya Kibantu.

 

TUMEKUWA tukichambua nadharia kuhusu chimbuko la lugha ya Kiswahili.

Katika makala iliyotangulia tuliangazia nadharia kuwa Kiswahili ni Kibantu. Tuliangazia maenezi mbalimbali ya Wabantu kihistoria yaliyowezesha kusambaa kwa Kiswahili ukanda wa Afrika Mashariki.

Mtawanyiko wa Pili 

Awamu hii ilitokea mwaka 1 KK. Kundi la Wabantu lililokuwa na maskani Kusini mwa Msitu wa Kongo lilitawanyika na kuenea eneo kubwa la Afrika ya Kati..

Awamu ya Tatu 

Kipindi kati ya mwaka 100 hadi 1100 BK kilishuhudia wimbila tatu la mtawanyiko uliotokana na ongezeko la watu na msongamano uliotokana na upungufu wa ardhi ya kilimo – ulisababisha kutawanyika kwaWabantu kutoka sehemu za Katanga kuelekea Kusini na Kaskazini-Mashariki.

Kundi hili la Wabantu ndilo liliingia nyanda za kati ya Afrika ya Mashariki katika karne ya kwanza na pili BK.Wabantu walioingia Afrika ya Mashariki waliendelea kugawanyika katika vikundi vidogovidogo kadiri walivyozagaa na muda kupita.

Baadhi ya vikundi hivi vilielekea upande wa Mashariki (sehemu ambayo sasa ni Kenya) mpaka kufikia Shungwayaya. Kulingana na fasihi simulizi, sehemu hii ya mabonde yenye rutuba ilikuwa baina ya Mto Juba huko Somalia na Mto Tana nchini Kenya.

Mnamo karne ya 5BK,Wabantu waliosakini Shungwaya walisambaa sehemu mbalimbali hasa za pwani ya Bahari Hindi. Kuhama huko kulisababishwa na majanga mbalimbali yakiwemo njaa kutokana na ukame, maradhi yakuambukiza, ukosefu wa ardhi yenye rutuba na msongamano wa watu.

Hata hivyo, tukio lililoharakisha uhamaji ni mashambulizi ya kabila la Wagalla.Uhamiaji kutoka Shungwaya ulitokea kwa mikondo na nyakati tofauti. Baadhi ya kikundi cha Wabantu walielekea upande wa Magharibi, huku wengine wakienda Kusini.

Kikundi kinachounda makabila ya Gikuyu, Wameru,Waembu na Wakamba walifuata Mto Tana na kuanzisha makaazi katika eneo linalouzunguka Mlima Kirinyaga au Kenya kama unavyojulikana leo hii.

Wasegeju nao walielekea Kusini na kukalia eneo baina ya pwani na milima yaUsambara. Kikundi kinachojiita Wataita kilianzisha makaazi kwenye milima ya Taita karibu na Mlima Kilimanjaro.

Mnamo karne ya 5BK,Wabantu waliosakini Shungwaya walisambaa sehemu mbalimbali hasa za pwani ya Bahari Hindi.

Kuhama huko kulisababishwa namajanga mbalimbali yakiwemo njaa kutokana na ukame, maradhi ya kuambukiza, ukosefu wa ardhi yenye rutuba na msongamano wa watu.

 

Marejeo:

Mehrabian na Ferris (1967). "Inference of Attitude from Nonverbal Communication in Two Channels". Katika: The Journal of Counselling Psychology Vol.31, 1967, pp.248-52.

Witzany, G. (2006 Plant Communication from Biosemiotic Perspective. Plant Signaling na Behavior 1 (4): 169-178