Nadharia za Urekebishaji Pamoja katika mawasiliano

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Tuesday, November 13  2018 at  07:24

Kwa Muhtasari

Urekebishaji Pamoja ni nadharia muhimu ya kuelezea vijidaraja vya mchakato wa mawasiliano.

 

NADHARIA za Urekebishaji Pamoja hufafanua mawasiliano kama mchakato wa ubunifu na unaobadilika badilika, unaoendelea wala si kubadilishana tu kwa habari.

Kwa mujibu wa mtaalamu Innis Harold watu hutumia njia mbalimbali kuwasiliana na njia watakayochagua kutumia itawapa uwezekano tofauti wa kuumba na kudumisha jamii (Wark, McKenzie 1997).

Katika ufafanuzi wake anatumia mfano maarufu kuhusu Misri ya kale na kuangalia jinsi walivyojenga wenyewe nje ya vyombo vya habari kwa aina tofauti za mawe na mafunjo.

Dhana mbili kutokana na mtazamo huu ni kama zifuatazo:

'Kufunga Nafasi (Space Binding)' – au mafunjo ni hali hii iliyowezesha kupitishwa kwa maandishi kutoka sehemu moja hadi nyingine na kuwezesha kufanyika kwa kampeni za kijeshi za mbali na utawala wa kikoloni.

'Kufunga Wakati (Time Binding)', - ni dhana nyingine mathalan kupitia ujenzi wa mahekalu na piramidi, wanajamii husika wanaweza kuendeleza mamlaka yao kizazi hadi kizazi.

Wataalamu wengi hawajifungi katika kuangazia tu mawasiliano ya binadamu. Kulingana na mtazamo huu kila mabadilishano ya habari au ishara kati ya viumbe vilivyo hai kwa kunakohusiha mtumaji na mpokeaji walio hai - kunaweza kuchukuliwa kama njia ya mawasiliano.

Mawasiliano ya wanyama yanaweza kuangaziwa kwa upana kwa kutazama masuala kadha katika taaluma ya ethnolojia.

Katika upeo wa juu zaidi kuna ubadilishanaji wa ishara kati ya seli za mwilini na mawasiliano ya kemikali kati ya viumbe asili kama vile bakteria na baadhi ya mimea.

Michakato hii yote ya mawasiliano huhusisha mitagusano inayoshirikisha ishara zilizo na utaratibu bainifu mbalimbali.

Mawasiliano ya wanyama yanahusisha tabia yoyote ya mnyama iliyo na athari ya sasa au baadaye kwenye tabia ya mnyama mwingine.

Kwa mtazamo mwingine,  mawasiliano ya binadamu yanaweza kujumlishwa kama mawasiliano ya wanyama yaliyoendelezwa.

Zoosemiotics – ni utafiti wa mawasiliano ya wanyama.

Anthroposemiotiki – Ni utafiti wa mawasiliano ya binadamu.

Soosemiotics imechangia pakubwa katika ukuzaji wa wa etholojia, biolojia jamii na taaluma kuhusu uwezo wa wanyama kutambua.

Ni dhahiri kwamba binadamu huwa wanaweza kuwasiliana na wanyama kama vile pomboo na wanyama wengine wanaotumika katika michezo ya sarakasi (circus).

Marejeo:

Mehrabian na Ferris (1967). "Inference of Attitude from Nonverbal Communication in Two Channels". Katika: The Journal of Counselling Psychology Vol.31, 1967, pp.248-52.

Witzany G (2008). Bio-Communication of Bacteria and their Evolutionary Roots in Natural Genome Editing Competences of Viruses. Open Evolution Journal 2: 44-54.