http://www.swahilihub.com/image/view/-/2605026/thumbnail/932754/-/1ylmenz/-/messi+flv.jpg

 

Chipukizi apania kuwa Messi Mkenya

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Wednesday, January 28  2015 at  15:29

Kwa Muhtasari

Katika umri wa miaka 16 Erickson Kamwaro ana matumaini ya kuwa mojawapo ya viunga wa kati wanaofahamika ulimwenguni.

 

KATIKA umri wa miaka 16 Erickson Kamwaro ana matumaini ya kuwa mojawapo ya viunga wa kati wanaofahamika ulimwenguni.
Lakini kwa sasa Ericson Kamwaro yungali mbali kabla ya kufikia kiwango cha kimataifa kwani kwa sasa anaichezea timu ya Makadara Juniors, viungani mwa jiji la Nairobi.
Mojawapo ya mataji ambayo ameshinda kama mchezaji wa timu hii ni kombe la Land Mawe, walilotwaa mwaka huu kama mchezaji wa timu ya wavulana wasiozidi miaka 17.
“Shindano hili liliandaliwa kwa minajili ya kuwasaidia vijana kuhepukana na matumizi ya madawa ya kulevya, halikadhalika uhalifu,” aeleza.
Pia wanashiriki katika shindano la Kariobangi ambalo bado linaelndelea.

“Shindano hili lilikatizwa kwa muda lakini tunatarajia kurejea uwanjani hii leo ambapo tilishinda mechi mbili za mwanzoni,” aeleza.
Kamwaro pia ni mwanafunzi wa shule ya upili ya St Partricks ambapo tayari yuko katika timu ya shule.

“Nilijumuishwa kawatika timu ya shule mwaka huu lakini hatujaweza kucheza kwani bado kuna mipango ya kuunda timu nzuri. Ifikiapo mwaka ujao tutakuwa tayari tumeanza kucheaza,” asema.
Kama wanasoka wengi alianza  kusakata kambumbu akiwa na umri mdogo.

Katika umri wa miaka minne alijiunga na timu ya wavulana wasiozidi miaka 10 katika timu ya Jerusalem, jijini Nairobi.

Baadaye alijiunga na timu ya Revelation mtaani humo humo kabla ya kuhama na kujiunga na timu yake ya sasa.
Ari yake ya kuwa mchezaji imechangiwa na wazazi wake abao mbali na kumpa motisha, walimfadhili kwa kumnunulia vifaa vya mazoezi.

Kadhalika anasema kuwa uchezaji wake pia umechangiwa na wanasoka mahiri kama vile Lionel Messi wa Barcelona na Christiano Ronaldo wa Real Madrid.
“Hawa ni wanasoka ambao wakiwa uwanjani hauna budi ila kutazama mchezo wao wa kupendeza na uliojaaa ustadi,”aeleza.
Kati ya changamoto ambazo zimekuwa zikirejesha nyuma jitihada zake za kujiimarisha katika mchezo huu ni ukosefu wa vifaa.

“Wazazi wangu hunisaidia lakini kuna wakati ambapo pengine wanakumbwa na majukumu mengine kiasi cha kuwa wanashindwa kuninunulia vifaa vyote,” asema.
Mbali na hayo pia analalmikia shida ya kupata majeraha ya kila mara ambapo mchezaji analazimika kugharamia matibabu mwenyewe.
Lakini hayo hayajazima Ndoto yake ya wakati mmoja kuichezea Sofapaka halikadhalika kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa.

“Pia natumai wakati mmoja kuichezea Chelsea, klabu ambayo naienzi kwa kutambua vipaji kutoka Afrika,” aongeza.