http://www.swahilihub.com/image/view/-/2605246/thumbnail/932882/-/w24qgx/-/odhis+flv.jpg

 

Chipukizi anayepania kumuiga mjombake 'Cantona'

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Wednesday, January 28  2015 at  18:28

Kwa Muhtasari

Anapania kufuata mfano wa aliyekuwa kiunga wa kati wa AFC Leopards na Harambee Stars, Eric ‘Cantona’ Ochieng ambaye pia ni mjomba wake.

 

ANAPANIA kufuata mfano wa aliyekuwa kiunga wa kati wa AFC Leopards na Harambee Stars, Eric ‘Cantona’ Ochieng ambaye pia ni mjomba wake.

Lakini huenda nyota ya Kayci Odhiambo ikang’aa hata zaidi hasa kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi mbili uwanjani, kama difenda na straika.


Katika umri wa miaka 14 pekee haina anajitahidi vilivyo kufanya vyema kama mwanasoka yeyote katika mitaa ya Nairobi hata anavyozidi kusubiri kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.


Wiki jana alishiriki katika shindano la Ligi ndogo Planet Cup kwa wavulana wasiozidi miaka 17, huku akijumuishwa katika kikosi cha kwanza cha timu ya Makadara Junior Academy.

“Ni mechi ambayo tulishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Dandora Indomitable,” mjini Nairobi.


Pia mwaka jana kama nahodha aliiongoza klabu hiyo katika fainali za Copa Cocacola, katika mechi iliyotoka sare dhidi ya JMJ Academy.

“Hata hivyo tulipoteza kutokana na tofauti ya mabao,” aeleza.


Pia amechaguliwa kujiunga na timu ya MYSA inayotarajiwa kwenda nchini Norway mwezi Juni kushiriki katika shindano la wiki tatu.
“Tayari nilianza mazoezi mwezi Desemba na mambo yakienda vyema basi nitakuwa mmoja wa watakaosafiri,” aeleza.


Kipaji chake kilianza akiwa angali mdogo huku akijiunga na klabu ya Makadara Junior akiwa katika darasa la tano. 

Hata hivyo umri wake haukumzuia kwani haikuwa muda kabla yake kujumuishwa katika kikosi cha wavulana wasiozidi miaka kumi.


Mchezo wake wa kupendeza ulimhakikishia nafasi katika kikosi cha shule ya msingi ya Rabai, mashariki mwa jiji la Nairobi pindi alipofika darasa la sita.


“Nikiwa shuleni tulishirki katika mashindano kadha na kufanya vyema lakini shindano la Orange miaka mitatu iliyopita halitanitoka
mawazoni,” aeleza.
Japo waliondolewa katika awamu ya mchujo, asema kuwa kushiriki katika shindano la haiba uya juu hivyo kulimpa moyo.
Akiwa katika darasa la sita alichaguliwa kama difenda bora katika shindano la Back to School.

Kadhalika miaka miwili iliyopita akiwa katika kikosi cha timu ya shule, walishiriki katika shindano la shule za msingi la Athi River lililojumuisha shule kadha mjini Nairobi.


Anasema msukumo wake wa kuwa mwanasoka ulichangiwa pakubwa na mojambake Cantona aliyekuwa akimuonyesha sidii zake akiwa uwanjani wakati huo akiwa mchezaji wa Ingwe na timu ya taifa,” aeleza.


Kadhalika anasema kuwa uchezaji wake umechangiwa pakubwa na kiungo mkabaji wa Bayern Munich na Ujerumani, Philipp Lahm
Matumaini yake ni wakati moja kuhusishwa katika kikosi cha Kogalo na hata kuichezea Barcelona, kando ya miamba kama Messi.