http://www.swahilihub.com/image/view/-/2605262/thumbnail/932900/-/5wpbshz/-/ken+flv.jpg

 

Kennon azungumzia kibao chake kipya

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Wednesday, January 28  2015 at  19:07

Kwa Muhtasari

Kwa mara ya nne mwaka wa 2014, produsa na msanii wa nyimbo za injili, Kennedy Otieno Liech al-maarufu amewapa mashabiki sababu ya kutabasamu.

 

KWA MARA ya nne mwaka wa 2014, produsa na msanii wa nyimbo za injili, Kennedy Otieno Liech al-maarufu amewapa mashabiki sababu ya kutabasamu.
Mtunzi huyu wa kibao ‘Bonga Points’ amezindua wimbo mpya kwa jina, 'Ni Wewe’, muziki ambao japo ulirekodiwa mwezi Aprili, ulizinduliwa rasmi mwishoni mwa mwaka wa 2014.
“Ilibidi kusubiri kutokana na hali siku hizi ambapo uzinduzi wa audio lazima uambatane na video ili wimbo ushabikiwe vilivyo,” asema.
Wimbo huu unawapa imani wanaokumbwa na changamoto za kila siku, huku hisia za kina za kidini zikijitokeza.
Katika kibao hiki, Kennon amemhusisha mwanamuziki chipukizi, Savatia ambapo sauti yake inasikika katika kiitikio cha wimbo huu.
Mwaka huu bila shaka umekuwa wa shughuli nyingi kwa Kennon hasa ikizingatiwa kuwa tayari amezindua vibao vingine vitatu kwa jina ‘This is Me’, ‘Spare Parts’ na ‘Alipenda Doh’ (Remix) ambapo amewahisisha wasanii wengine sita.
Kwa ujumla, hiki ni kibao cha Kennon cha sita tangu ajitose rasmi kwa muziki mwaka wa 2010. Itakumbukwa kuwa mwaka huo huo, kwa ushirikiano na produsa mwenzake, Luminas, walizindua kibao ‘Kaza Kamba’, na kuwapelekea kupata taji la ushirikiano bora wa mwaka katika tuzo za Mwafaka.
Kama produsa, amewarekodia nyimbo wasanii kama vile Alahola Synonimaous kwa kibao chake “Miss Mboch”, Pace, Kayvo K-force, Ace the don na Tetete kwa kutaja wachache.
‘Ni Wewe’ imerekodiwa katika Climax Studio, kwa ushirikiano na Luminas ambaye ni produsa mshiriki katika studio hiyo.