http://www.swahilihub.com/image/view/-/2607278/thumbnail/934296/-/10nu1am/-/sweep+flv.jpg

 

Watu 2 washinda Sh1.35 milioni

Na SAMMY KIMATU

Imepakiwa - Friday, January 30  2015 at  11:48

Kwa Muhtasari

Wakenya wawili wamejawa na faraja baada ya kushinda Sh1.35 milioni katika shindano la Lotto.

 

MKULIMA kutoka eneo la Gichugu katika Kaunti ya Kirinyaga na meneja wa mipagilio (logistics manager) katika kampuni moja lililoko Eneo la Viwandani Kaunti ya Nairobi leo walitangazwa washindi wa Sh1.35 milioni katika shindano la Lotto 636 linaloendeshwa na Shirika la Bahari Nasibu Nchini  (Kenya Charity Sweepstake).

Akiongea wakati wa kuwakabidhi cheki, meneja wa uhusiano mwema wa Kenya Charity Sweepstake, Bw Peter Njoroge alisema wawili hao watagawana zawadi hiyo kwa mujibu wa sheria za mchezo huo.

Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za shirika hilo hapa katikatiu mwa jiji la Nairobi.

Bw Njoroge alisema Ikiwa kutaibuka mshindi zaidi ya mmoja, washindi, haijalishi ni wagapi, bila shaka watagawana zawadi hiyo pamoja.

Bw Harun Muchira Kiura mwenye umri wa miaka 47 na baba wa watoto watatu ni mkulima kutoka Gichugu huku Bw Kenneth Ndeva Asega mwenye umri wa miaka 50 na baba wa mtoto mmoja akiwa meneja katika kampuni la Kamongo lililoko kwenye Eneo la Viwandani Nairobi.

Bw Muchira alisema atatumia pesa hizo kupanua kazi yake ya ukulima naye Bw Asega akisema atatunua ploti Kakamega kisha ajenge nyumba za kukodisha.