http://www.swahilihub.com/image/view/-/2607428/thumbnail/934359/-/ipl22q/-/Shaniqua+flv.jpg

 

Shaniqwa aazimia kumpiku Vera Sidika

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Friday, January 30  2015 at  12:53

Kwa Muhtasari

Ni mmoja wa chipukizi wanaonuia kuuteka ulimwengu wa wasosholaiti nchini, angaa kulingana na nafasi anayoiigiza katika kipindi cha televisheni cha Jameni.

 

NI MMOJA wa chipukizi wanaonuia kuuteka ulimwengu wa wasosholaiti nchini, angaa kulingana na nafasi anayoiigiza katika kipindi cha televisheni cha Jameni.
Katika kipindi hiki anafahamika kama Shaniqwa ambapo anaashiria binti anayetamani sana kuwa mwanasosholaiti na ambaye anajiamini kuwa mrembo zaidi, kiasi cha kuwapa wengine katika ulingo huu mfano Vera Sidika, ushindani mkali.

Utundu na usumbufu wake kwa upande mwingine unajitokeza dhahiri hasa pindi anapaofungua mdomo wake kuzungumza, huku yake mengi yanayojumuisha mavazi mafupi na yaliyombana, nywele ndefu za kubandika na viatu vya visigino virefu ajabu vikiwa baadhi ya vitambulisho vyake.

Wengi wanaohoji kuwa ni jambo linalomsaidia kutokeza muonekano halisi unaohusishwa na mabinti wa aina hii katika jamii.
Lakini hiyo ni picha tofauti unapokumbana na kaka anayeigiza nafasi hii kwani licha ya ucheshi wake kudhihirika hata katika maisha halisi, Kelvin Mwangi ni mpole na mtulivu, tofauti kubwa ambayo yaweza waacha wengi vinywa wazi kwa kujiuliza ni vipi anavyojibadilisha mara moja?
Huenda hiyo ni mojawapo ya sababu ambazo zinamfanya kuigiza vizuri katika nafasi hii ambayo impeempa umaarufu kiasi cha wengi kusahau kuwa amewahi igiza katika vipindi kadha kabla ya hapa kama vile Mheshimiwa, Comedy Club na Heroes Mtaani.