http://www.swahilihub.com/image/view/-/2810808/thumbnail/1073912/-/wd7ho5/-/Eqwiti.jpg

 

Equity kupokea dola 148 milioni kutoka AfDB

Na SALATON NJAU

Imepakiwa - Monday, July 27  2015 at  16:55

Kwa Muhtasari

Equity kupokea dola 148 milioni kutoka AfDB

 

Benki ya Equity na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimetia saini makubaliano ya dola $148milioni ya mkopo wa kuwezesha kutolewa kwa mikopo kwa wafanyabiashara wa mashirika madogo ya kibinafsi katika sekta muhimu za kiuchumi nchini Kenya na Afrika Mashariki. Mkopo huo kwa Benki ya Equity unatarajiwa kuongeza maendeleo ya sekta binafsi nchini Kenya kupitia ufadhili wa miradi.