Maana, sifa na umuhimu wa vikoa vya maana katika Semantiki na Mawasiliano

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Tuesday, March 6  2018 at  15:05

Kwa Muhtasari

Vikoa vya maana humaanisha seti za maana ya uhusiano uliopo wa fahiwa mbalimbali.

 

Vikoa vya maana

Ni seti ya mahusiano. Maneno hayo katika kitengo kimoja yannaweza kuhusiana kwa namna mbalimbali, kwa mfano unyume, usinonimia, uhiponimia, umeronimia na kadhalika. Kwa mukhtasari, haya ni mahusiano ya kifahiwa.

Usinonimia unaweza kutumika kueleza maana ya maana kwa namna mbili jinsi ifuatavyo:

i. Kutumia ujuzi wa sinonimia - Kwa mfano; mtu mmoja labda hajui maana ya wadhifa; ili kumsaidia utamwambia cheo. Hapa utakuwa umetumia ujuzi wa sinonimia katika kuelezea maana ya maana.

ii. Kinyume cha sinonimia - Au unaweza kumweleza mtu maana ya neno kwa kumweleza kinyume chake.

Kwa mfano; anataka kujua nadra; unamweleza kinyume chake tu.

Sifa ya vikoa vya maana

Hakuna sifa maalumu katika kuanza. Unaweza kuanza na neno lolote katika kundi husika. Kwa mfano nikitaka kusema wanyama: naweza kuanza na neno lolote kama vile simba, chui na kadhalika.

Umuhimu wa vikoa vya maana

i. Husaidia kujua maana ya maneno katika lugha. Kwa mfano, ili uweze kujua kikoa cha wanyama lazima ujue baadhi ya wanyama.

ii. Husaidia katika kujifunza lugha. Kwa mfano mtoto anapojifunza rangi huanza na kikoa cha rangi nyeupe na nyeusi.

iii. ikoa vya maana husaidia kuchanuza maana katika lugha.

iv. Husaidia kuonesha umbo la wingi. Kwa mfano, badala ya kusema kikoa cha tunda tunasema kikoa cha matunda - yaani umbo la wingi ni la msingi sana katika vikoa vya maana.

v. Hurahisisha mawasiliano au ukipenda hukoa huokoa muda. Kwa mfano ukifika sokoni unaweza kusema: Je, kuna mboga za majani?‘ yaani badala ya kuuliza iwao kuna mchicha, mrenda, mgagani, tembele na kadhalika.

vi. Hufanikisha shughuli za wanafunzi wa leksikografia.

CHANGAMOTO ZA VIKOA MAANA KATIKA MAWASILIANO

i. Kuna baadhi ya vikoa maana ambavyo havina idadi maalum kwa mfano: idadi ya siku kwa wiki, wanyama na kadhalika.

ii. Maneno katika baadhi ya vikoa maana huwa na uhusiano wa karibu sana kiasi kwamba ni vigumu sana kuyaelewa. Kwa mfano chui na dubu

iii. Dhana hizi za vikoa maana ziko akilini mwa watu tu.

Marejeo

1. Massamba P. B. D (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.

2. Mdee, J. S (1997), Nadharia na Historia ya Leksikografia, Dar es Salaam:TUKI.

3. Morris, Charles W. (1971), Writings on the general theory of signs, The Hague: Mouton