Vitengo vikuu katika nadharia ya mawasiliano

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Monday, November 12  2018 at  08:18

Kwa Muhtasari

Viambajengo vikuu na vya kimsingi vya mawasiliano ni ujumbe, chanzo, aina, na mfumo au njia.

 

KIMSINGI, mawasiliano yanahusisha viambajengo vikuu vinavyoainishwa ifuatavyo:

  1. Ujumbe – Ni mambo ya aina gani yanayosemwa
  2. Chanzo / mtumaji / Msemaji au mfumbaji – ni anayetuma ujumbe
  3. Aina – ni ujumbe wa aina gani?
  4. Mfumo au njia  - ujumbe huo unatumwa kupitia njia gani?

Kituo, unapokwenda / mpokeaji / mlengwa – ujumbe unakwenda wapi ni nani anayepokea ujumbe lengo au nia ya ujumbe – hiki ni kipengele cha kipragramatiki.

Mawasiliano yanahusisha vitendo vinavyotunukia maarifa na tajriba, kupatia mawaidha na amri, na kuuliza maswali.

Matendo haya yanaweza kuchukua sura nyingi, katika mojawapo ya njia mbalimbali za mawasiliano. Sura hizi hutegemea uwezo wa kikundi kinachowasiliana.

Maudhui na sura za mawasiliano hutumika pamoja kukamilisha ujumbe unaotumwa mahali.

Hadhira lengwa inaweza kuwa msemaji mwenyewe,mtu mwingine au kiumbe kingin au hata kikundi kingine.

Vilevile, mawasiliano yanaweza kuonekana kama mchakato wa kusambaza habari unaoongozwa na vitengo vitatu vya sheria za elimu ishara jinsi ifuatavyo:

  1. Kitengo cha kisintaksia – Sifa rasmi za ishara na viashiria.

  2. Kitengo cha kipragmatiki – kinahusika na mahusiano kati ya ishara au maneno na watumiaji wake.

  3. Kitengo cha kisemantiki – uhusiano kati ya ishara na viashiria vinavyowasilisha.

Kwa mantiki hiyo, mawasiliano ni mwingiliano wa kijamii ambapo angalau vitu au watu wawili wanaotagusana hutumia seti moja ya ishara na seti moja ya kanuni za elimu ishara.

Kanuni hizi zinazozingatiwa wakati mwingine huwa zinapuuza mawasiliano ambayo hutokea ghafla bila kupangiwa mathalan mawasiliano yanayohusisha mtu na nafsi yake kupitia kwa shajara au mazungumzo-nafsi.

Habari au maudhui kama vile ujumbe katika lugha asilia hutumwa katika njia fulani kama lugha ya mazungumzo kutoka kwa msemaji kwa mpokeaji.

Msemaji na mpokeaji huwa wameunganishwa kwa wakati mmoja. Mfano mmoja wa mawasiliano ni kama tendo usemi.

Namna ya kutafsiri ujumbe ya msemaji inaweza kuwa tofauti na ya msikilizaji kulingana na desturi na tamaduni za eneo la wanajamii au jinsia walilomo, au jinsia; mambo ambayo yanaweza kuathiri ujumbe uliokusudiwa.

Uwepo wa kelele za mawasiliano katika  njia inayotumiwa, mapokezi na ufumbuaji wa ujumbe unaweza kuathiriwa, hivyo basi tendo usemi linaweza kutofikia matokeo yaliyotarajiwa.

Marejeo: 

Mehrabian na Ferris (1967). "Inference of Attitude from Nonverbal Communication in Two Channels". Katika: The Journal of Counselling Psychology Vol.31, 1967, uk.248-52.

Witzany, G. (2006 Plant Communication from Biosemiotic Perspective. Plant Signaling na Behavior 1 (4): 169-178.

Witzany, G. (2007 Applied Biosemiotics: Fungal meddelande. Katika: Witzany, G. (Ed). Biosemiotics in Transdisciplinary Contexts. Helsingfors, Umweb, uk. 295-301.