http://www.swahilihub.com/image/view/-/4344458/medRes/1909598/-/aq7ajhz/-/zozana.jpg

 

Viziada lugha (paralanguage)

Wapenzi

Uchungu wa mapenzi hakuna asiyejua. Picha/HISANI 

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Friday, November 2  2018 at  09:59

Kwa Muhtasari

Viziada lugha (paralanguage) ni vipengele vya mawasiliano kwa ishara ambavyo huhusisha ubora wa sauti, hisia na mitindo ya kuzungumza, ikiwa pamoja na sifa za kiarudhi kama vile mdundo, lafudhi na msisitizo.

 

VIZIADA LUGHA (PARALANGUAGE)

VIZIADA LUGHA (paralanguage) ni vipengele vya mawasiliano kwa ishara ambavyo huhusisha ubora wa sauti, hisia na mitindo ya kuzungumza, ikiwa pamoja na sifa za kiarudhi kama vile mdundo, lafudhi na msisitizo.

Isitoshe, matini zilizoandikwa zina vipengele vya mawasiliano kwa ishara kama vile mtindo wa kuandika, mpangilio wa maneno au matumizi ya hisia.

Aina nyingine za mawasiliano ya viziada lugha ni kama vile telegrafia ambapo ishara hupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia tofauti. Ishara hizi zinaweza kuwa viwakilishi vya maneno, vifaa au makadirio tu.

Mtaalamu GW Porter anagawanya mawasiliano ya kutumia ishara katika makundi manne jinsi ifuatavyo:

Kimwili. Hii ni aina ya mawasiliano ya binafsi. Mawasiliano hayo yanahusisha ishara za uso, toni ya sauti, kugusa, kunusa, na miondoko ya mwili.

Ujumi. Hii ni aina ya mawasiliano ambayo hufanyika kupitia njia za ubunifu:mathalan kucheza ala ya muziki, densi, uchoraji na uchongaji.

Ishara. Hii ni aina ya mawasiliano, ambayo inajumuisha matumizi ya bendera za ishara, milio 21 ya bunduki, pembe, ving’ora na kengele.

Kiashiria. Hii ni aina ya mawasiliano ambayo inatumia alama za kidini, hadhi, au za kujenga nafsi.

Sifa zisizobadilika

Umbali. Umbali mtu mmoja anaosimama kutoka kwa mtu mwingine kwa kawaida huwasilisha ujumbe fulani. Katika baadhi ya tamaduni hii ni ishara ya mvuto, na kwa wengine inaweza kuonyesha hadhi au umuhimu wa ujumbe unaopitishwa.

Namna ya kujiwasilisha. Watu wanaweza kujiwasilisha kwa njia mbalimbali: uso kwa uso, ubavu ubavu, au hata wakifuatana. Kwa mfano, watu walio na ushirikiano kuna uwezekano watakaa ubavu kwa ubavu na washindani wakati mwingi hutazamana.

Namna ya kukaa. Kwa kawaida mtu anaweza kuwa amelala chini, ameketi, au amesimama. Hivi si vipengele vya mkao vinavyowasilisha ujumbe.

Mgusano wa kimwili. Kusalimiana kwa mikono, kugusana, kushikana, kukumbatiana, kusukumana, au kupiga kofi mgongoni haya yote huwasilisha ujumbe. Huwa yanaashiria urafiki au hisia za (au ukosefu wa) mvuto.